Mwezi tatu Shabani iliangaza nuru ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi tatu Shabani ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s), aliyezaliwa mwaka wa tatu Hijiriyya katika nyumba ya Utume na mashukio ya malaika.

Imamu (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina ndani ya nyumba ya wazazi wake jirani na nyumba ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na msikiti wa Mtume ambao ni miongoni mwa sehemu takatifu katika uso wa Dunia, na amelelewa katika miguu ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akajifunza ukarimu, ushujaa na utukufu hadi akajulikana (a.s) kwa tabia njema na kufanana na babu yake (s.a.w.w) pamoja na kaka yake Imamu Hassan (a.s).

Shekh Tusi amepokea kwa vyanzo vinavyo aminika kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) anasema: (…Asmaa anasema: Pindi Fatuma alipomzaa Hussein (a.s), alikuja Mtume (s.a.w.w) akasema: Niletee mwanangu ewe Asmaa, nikampa akiwa amefunikwa kitambaa cheupe, akamfanyia kama alivyo mfanyia Hassan (a.s), kisha akasema: Akalia Mtume (s.a.w.w) halafu akasema: Hakika utauwawa, Ewe Mola mlaani atakaemuuwa. “Akaniambia”: usimuambie Fatuma jambo hili, akasema: Ilipo fika siku ya saba akaja Mtume (s.a.w.w) akasema: Niletee mwanangu, nikampelekea, akamfanyia hakika kwa kuchinja mbuzi, na akamnyoa nywele na kutoa sadaka ya fedha kwa uzito wa nywele hizo, halafu akamuweka miguuni kwake na akasema: Ewe Abu Abdillah kuuwawa kwako kunaniumiza, kisha akalia, Asmaa akasema: Naapa kwa haki ya baba yangu wewe na mama yangu, ulifanya kama vivi katika siku ya kwanza, kwa nini? Akasema: Namlilia mwanangu atauwawa na kundi ovu miongoni mwa kizazi cha Umayya Mwenyezi Mungu awalaani na mimi sitawaombea siku ya kiyama, atauwawa na mtu anaedai yupo kwenye Dini, na anamkufuru Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha akasema: Ewe Mola nakuomba kwa watoto hawa (Hassan na Hussein a.s) kama alivyo kuomba Ibrahim kwa kizazi chake, ewe Mola nawapenda na ninampenda atakaewapenda na mlaani atakae wachukia mbinguni na aridhini).

Imepokewa kutoka kwa Shekh Kuleini katika kitabu cha Usulu-Kafi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hussein hakuwahi kunyonya kwa Fatuma (a.s) wala kwa mwanamke yeyote, alikua anapelekwa kwa Mtume (s.a.w.w) anamuweka kidole chake mdomoni ananyonya na kushiba kwa siku mbili hadi tatu, muili wa Hussein (a.s) ulijengeka kutokana na muili wa Mtume (s.a.w.w), wala hakuna aliyezaliwa kamili kwa ujauzito wa miezi sita ispokua Nabii Issa mwana wa Maryam na Hussein bun Ali (a.s)).

Mtume (s.a.w.w) alimpa kipaombele maalum Imamu Hussein (a.s), jambo lililo onyesha utukufu wake tangu utotoni, alikuwa (s.a.w.w) anausia kumpenda Imamu Hassan na Hussein (a.s), anasema: (Atakae mpenda Hassan na Hussein nitampenda, na nitakae mpenda atapendwa na Mwenyezi Mungu, na atakaependwa na Mwenyezi Mungu ataingizwa peponi, atakae wachukia nitamchukia, na nitakae mchukia atachukiwa na Mwenyezi Mungu, na atakaechukiwa na Mwenyezi Mungu ataingizwa motoni milele), anasema (s.a.w.w): (Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussein, Mwenyezi Mungu anampenda anaempenda Hussein, Hussein ni miongoni mwa wajukuu).

Hivi ndio alivyokua Imamu Hussein (a.s) mbele ya babu yake Mtume mtukufu (s.a.w.w) alikua anafanana naye kwa sura na tabia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: