Waziri wa viwanda wamesema kuwa: Miradi ya Ataba tukufu inamafanikio makubwa

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri siku ya Jumatano (3 Shabani 1442h) sawa na tarehe (17 Machi 2021m), waziri wa viwanda Sayyid Manhal Azizi Alkhabbaazi ametembelea Atabatu Abbasiyya, kuangalia huduma mbalimbali zinazo tolewa na Ataba tukufu.

Baada ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), waziri amekutana na katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi.

Mheshimiwa waziri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumepata utukufu wa kutembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na viongozi wake, kikao kimekuwa na faida kubwa kwani tumebadilishana mawazo na kuangalia faida ya viwanda katika mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Tumejadili pia namna ya kunufaika na uzowefu wa Atabatu Abbasiyya katika kuboresha viwanda vyake, kwani mafanikio ya miradi ya Atabatu Abbasiyya ni somo kubwa kwa taasisi zetu za viwanda”.

Naye mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi akasema kuwa: “Leo tumetembelewa na Mheshimiwa waziri wa viwanda kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wizara”, akasema: “Mheshimiwa waziri amevutiwa na miradi ya Ataba hasa katika sekta ya viwanda na amepongeza bidhaa zinazo tengenezwa na viwanda hivyo”.

Hasanawi akasema kuwa: “Mheshimiwa waziri ametoa wazo la kuanzisha tawi la wizara katika mkoa wa Karbala, litakalo shughulikia mambo yote ya viwanda, kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo katika mkoa huu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: