Mwezi nne Shabani dunia ilinawirika kwa kuzaliwa mwezi wa bani Hashim

Maoni katika picha
Siku kama ya leo alizaliwa mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s) alama ya undugu, uaminifu na kujitolea, alizaliwa mwezi nne Shabani mwaka wa 26 Hijiriyya, mazazi yake yalikua na umaalum wake, dunia ilijaa shangwe na furaha, nuru yake iliangazia dunia.

Mji wa Madina ulijaa furaha ukiongozwa na wanafamilia ya Hashimiyyu Al-Alawiyyu, kwa kuzaliwa mwezi wao ungáao, unao angazia mbingu ya dunia utukufu wake, alikuwa ni mtoto wa kwanza wa bibi mtukufu Ummul-Banina (a.s), kwa kuzaliwa kwake ukawa umezaliwa uaminifu na kujitolea, hakika alikuwa kielelezo bora kwa kuenzi undugu.

Kiongozi wa waumini (a.s) alipopewa taarifa ya kuzaliwa kwake, alienda haraka nyumbani na alipo fika alimbeba na kumbusu, kisha akamfanyia taratibu za kisheria, akamuadhinia kwenye sikio la kulia na kukim kwenye sikio la kushoto, hakika sauti ya kwanza kuingia katika masikio yake ni sauti ya baba yake kiongozi wa waumini na wachamungu duniani, sauti isemayo: “Allahu Akbaru…”, “Laa-Ilaaha Ila-Llaah”. Maneno hayo matukufu ambayo ndio ujumbe wa mitume na wimbo wa wachamungu yaliingia katika akili ya Abulfadhil Abbasi na kujikita ndani ya dhati yake, hadi ikawa ndio sifa yake kuu, akaishi akilingania maneno hayo katika uhai wake wote na akauwawa kwa ajili ya maneno hayo.

Siku ya saba tangu kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), kiongozi wa waumini (a.s) alinyoa nywele zake, na akatoa sadaka kwa masikini ya dhahabu au fedha kwa uzito wa nywele hizo na akamfanyia hakika, kama alivyo fanya kwa Hassan na Hussein (a.s) katika kutekeleza sunna ya Mtume wa kiislamu.

Kiongozi wa waumini (a.s) akampa jina la (Abbasi) mtoto wake, alikuwa anajua kuwa atakua jemedari wa kiislamu, atakuwa chukizo katika uso wa mtu muovu, na furahisho kwa mtu mwema. Hakika habari kuhusu Abulfadhil Abbasi (a.s) ni nyingi, haziwezi kuisha wala haziandikiki kwa mistari hii michache, ananafasi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, tumeandika haya machache kwa muhtasari katika kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: