Kuanza shindano la (miezi ya uongofu)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kwa shindano la kielimu kwa njia ya mtandao lililopewa jina la (miezi ya uongofu), nalo ni kongamano la kielimu linahusu kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaadi –a.s-), shindano hili linahusu mazazi hayo, kutakuwa na maswali mbalimbali kuhusu watu hao watakatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim, akasema: “Hili ni moja ya mashindano mengi yaliyoratibiwa na kituo chetu katika kumbukumbu za matukio ya Dini likiwemo hili, aidha ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Hili ni shindamo maalum kwa wanawake, na zimeandaliwa zawadi za washindi watatu, baada ya kupigiwa kura majibu sahihi kama yatakua zaidi ya matatu, majibu yote yatawasilishwa katika kamati ya majaji kwa ajili ya usahihishaji na kupanga matokeo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: