Kutandika kapeti jipya katika milango inayoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi, wametandika zulia kwenye milango yote inayo ingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), aina maalum kulingana na ukubwa wa kila mlango, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Alawiyya miongoni mwao mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s), na kufanya iwe na muonekano mzuri unao endana na kila mlango.

Makamo rais wa kitengo tajwa Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ubadilishaji wa mazulia ya milangoni hufanywa kila baada ya muda fulani na kwa kuzingatia hali ya mazulia hayo, watumishi wetu kwa kushirikiana na watumishi wa idara ya ushonaji pamoja na kitengo cha uangalizi wa majengo ya kihandisi, tumetandika mazulia mapya baada ya kuchukua vipimo vya kila mlango, hatua ya kwanza tumetandika katika eneo la mlango wa Kibla na Imamu Hassan (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya mlango wa Kibla imetandikwa kuanzia mlangoni hadi kwenye haram tukufu, na mlango wa Imamu Hassan (a.s) umetandikwa hadi kwenye haram”.

Kumbuka kuwa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kinajukumu la kutandika miswala na kuiosha kila baada ya muda fulani, kwa ajili ya kulinda uzuri wa haram tukufu na kudumisha usafi ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: