Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya unatoa pongezi katika kumbukumbu ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi mbele ya malalo yake takatifu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na Ustadh Fadhili Auzu ukiwa na wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo vyake, umetembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoa pongezi za maadhimisho haya matukufu, ambayo kumbukumbu yake inasadifu siku ya mwezi nne Shabani.

Ugeni huo umepokewa na ndugu zao watumishi wa malalo hiyo na wajumbe wa kamati kuu ya Ataba takatifu, na marais wa vitengo na watumishi wake, wakapeana pongezi kwa maadhimisho haya matukufu, huku mikono ya watumishi wa Atabatu Husseiniyya ikiwa imebeba mauwa waliyo kuja kuyaweka juu ya dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), na wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alipe amani na utulivu taifa la Iraq na raia wake, awaondolee mabalaa yote na kuwatunuku afya na amani na awaepushe na janga la Korona.

Baada ya hapo wakaenda katika ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya, na wakapokewa na katibu mkuu wa Ataba hiyo Mhandisi Muhammad Ashiqar, wakabadilishana mawazo kuhusu maadhimisho haya na wakasisitiza kuwa iwe chachu ya kuhuisha ahadi ya kuitumikia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: