Kuanza kongamano la kuchomoza miezi ya kielimu

Maoni katika picha
Alasiri ya Alkhamisi (4 Shabani 1442h) sawa na (18 Machi 2021m), kongamano la kielimu katika kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya limeanza chini ya anuani isemayo (Kuchomoza miezi.. kuhuisha mwenendo wa Mtume mteule na kizazi chake kitakatifu) na kauli mbiu inasema: (Baina ya Madina na Karbala harakati ya fikra na utoaji), linalo simamiwa na jumuiya ya kielimu Al-Ameed kwa kushirikiana na muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika nchi za ulaya, pamoja na chuo kikuu cha kiislamu cha Lebanon, kongamano limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom).

Baada ya Quráni ya ufunguzi iliyo somwa na Muslim Aqiil Shabaki, ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, uliowasilishwa kwa niaba yake na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Dokta Ahmadi Ridhwa Husseini.

Halafu ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi, ulio wasilishwa na Dokta Mushtaqu Abbasi Muan.

Baada ya hapo masikio ya wahudhuriaji yakaburudishwa kwa mashairi yaliyosomwa na Dokta Ahmadi Khiyali na Ali Swafaar, mashairi yaliyo elezea tukio hili takatifu na mapenzi ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Kisha vikaanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti, wasomi wa hauza na sekula kutoka ndani na nche ya Iraq, wamewasilisha mada zao kuhusu mwenendo wa miezi ya Alawiyya mitukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: