Kikao cha uwasilishaji wa mada za kitafiti kimeongozwa na Dokta Ali Mislawi, alifundua kwa kushukuru ushiriki wa watafiti katika kongamano hili, sambamba na kuishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ulezi wake katika harakati hii.
Mada zilizo wasilishwa ni:
- - Mada ya kwanza: (Kujitolea na siri ya utendaji kwa Ahlulbait –a.s-) imewasilishwa na Dokta Muhammad Abdallah/ kutoka chuo kikuu cha kiislamu cha Lebanon.
- - Mada ya pili: (Mwenendo wa Imamu Sajjaad na mwanae Baaqir –a.s- katika malezi na elimu) imewasilishwa na Dokta Karim Hussein Naaswihi/ kutoka jumuiya ya kielimu Al-Ameed.
- - Mada ya tatu: (Abbasi –a.s- mfundishaji wa ubunifu na elimu) imewasilishwa na Dokta Shekh Mahadi Gharuwi/ kutoka chuo kikuu cha kiislamu cha Lebanon.
- - Mada ya nne: (Athari ya kuzaliwa miezi mitatu katika masomo ya kihistoria na kijamii) imewasilishwa na Dokta Daudi Zubaidi/ kutoka chuo kikuu cha Al-Ameed.