Kongamano la kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya limehitimisha ratiba yake na kuweka maazimio

Maoni katika picha
Kongamano la kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya limehitimisha ratiba yake na kuweka maazimio, lilikuwa na uwasilishaji wa mada nyingi za kielimu.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na rais wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Mushtaqu Abbasi Muan, amesoma maazimio yaliyo andaliwa na kamati ya maandalizi, miongoni mwa maazimio hayo ni:

  • 1- Kongamano hili lifanywe kila mwaka.
  • 2- Kongamano lifanywe kwa kushirikiana na taasisi za kielimu kutoka nchi tofauti, nchi moja isirudie marambili mfululizo ili kuwezesha ushiriki wa nchi nyingi zaidi.
  • 3- Yaanze maandalizi ya kongamano lijalo kwa kuunda kamati mbili wiki moja baada ya kumaliza kongamano, ili kupata muda mrefu wa matangazo na kutoa nafasi ya kutosha kwa watafiti wa kielimu watakao shiriki kwenye kongamano.

Kongamano likahitimishwa kwa kuwapa zawadi watafiti walioshiriki kuwasilisha mada.

Kumbuka kuwa kongamano limefanywa siku ya Alkhamisi (4 Shabani 1442h) sawa na (18 Machi 2021m) chini ya anuani isemayo: (Kuchomoza miezi.. kuhuisha mwenendo wa Mtume mteule na Aali zake watakatifu), na kauli mbiu isemayo: (Muamko wa kielimu kati ya Madina na Karbala) chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Al-Ameed kwa kushirikiana na muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika nchi za ulaya pamoja na chuo kikuu cha kiislamu cha Lebanon.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: