Kuzaliwa kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi tano Shabani mwaka wa 38 hijiriyya mji wa Madina ulinawirika kwa kuzaliwa Imamu wa nne miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), Imamu Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Shekh Mufid anasema katika kitabu chake cha (Irshaad): Ali bun Hussein alikuwa mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu kwa elimu na vitendo baada ya baba yake, akasema: Imepokewa kutoka kwa wanachuoni kuwa alikuwa na elimu isiyo elezeka, yamepokewa kutoka kwake mafundisho mengi sana, mawaidha, dua utukufu wa Quráni, halali na haram na mengineyo mengi yanayo julikana katika ulimwengu wa wasomi.

Mama yake ni bibi Shahazanani binti wa Yazdajurd bun Shahriyaar bun Kisra, inasemekana kuwa jina lake ni Shaharubanu, na mke wake ni bibi Fatuma mtoto wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), laqabu zake (a.s) ni: Zainul-Aabidina, Sayyid Al-Aabidina, Sajjaad, Dhu-Thaqnaat, Imamu Mu-uminina, Zaahid, Amiinu, Mujtahidi, Azakiy… na mashuhuri zaidi ni Zainul-Aabidina. Na kuniya yake ni Abu Muhammad, Abu-Hassan, Abu-Hussein na Abu Qassim…

Riwaya zinaonyesha kuwa siku aliyo zaliwa (a.s) babu yake kiongozi wa waumini au mwanae Imamu Hussein (a.s) alimfanyia taratibu za kisheria, alimuadhinia kwenye sikio la kulia na akamsomea Iqama kwenye sikio la kushoto, adhana hiyo ilijikita katika moyo wake na kuwa msingi wa uchamungu wake, ilikuwa ukumbusho hai uliomuwezesha kutenda wema.

Jambo la kwanza alilosikia Imamu Zainul-Aabidina katika maisha yake ni sauti ya (Allahu Akbaru) nayo ilijiandika katika moyo wake, na siku ya saba tangu kuzaliwa kwake, baba yake alimfanyia hakika kwa kumchinjia mbuzi na akamnyoa nywele zake kisha akatoa sadaka ya fedha au dhahabu kwa uzito wa nyele hizo, kama ilivyo sunna tukufu ya kiislam.

Aliishi (a.s) miaka hamsini na saba takriban, na miaka miwili au minne katika hiyo aliishi chini ya uangalizi wa babu yake Ali (a.s), kisha akaishi chini ya Ammi yake Hassan na baba yake Hussein (a.s) wajukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), alijifunza elimu ya Mtume na maadili ya Ahlulbait watakatifu kutoka kwao.

Akawa ni Imamu wa Dini na kinara wa elimu na rejeo wa hukumu za kisheria, akawa kiigizo chema cha unyenyekevu na uchamungu, waislamu wote wanakubaliana kuhusu ukubwa wa elimu yake na msimamo wake na jinsi watu walivyo ongoka chini ya utawala wake.

Katika zama za Uimamu wake alikutana na watawala wa Umawiyyina wafuatao: Yazidi bun Muawiya, Muawiya bun Yazidi, Marwan bun Hakamu, Abdulmaliki bun Marwan na Walidi bun Abdulmaliki.

Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikuwepo katika siku ya Ashura, yalikuwa ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuilinda familia ya Mtume (s.a.w.w) na kuifanya dunia isibaki bila wao, ndipo Imamu (a.s) akapata ugonjwa mkali sana, hakuweza kusimama wala kutembea, hakuweza kupigania Dini siku hiyo wala kumlinda baba yake Imamu Hussein (a.s) na kuuwawa sehemu ile, hakika ilikua ni siri ya kuendeleza tukio la Ashura na kufanya lisifutike.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: