Maahadi ya Quráni tawi la wanawake imefanya hafla ya kupongeza wahitimu wa semina ya (Mnyweshaji wenye kiu) na (Zaakiyaatu)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya kuhitimu semina mbili za (Mnyweshaji wenye kiu) na (Azaakiyaatu), baada ya kufaulu mitihani ya mwisho iliyo tolewa na Maahadi, semina zililenga kuboresha usomaji wa Quráni ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na semina za kuhifadhi Quráni tukufu.

Kiongozi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake bibi Manaar Jaburi amesema kuwa: “Kunaongezeko la idadi ya wanafunzi wa Quráni tukufu”.

Akasisitiza kuwa: “Milango ya Maahadi ipo wazi daima kwa ajili ya kupokea wasichana wanaopenda kujifunza hukumu za usomaji wa Quráni hususan wasichana wanaoishi katika mkoa wa Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: