Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanaendelea na harakati ya kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mkoa wa Waasit, wanaendelea kupambana na janga la virusi vya Korona, kufuatia ongezeko la maambukizi katika mkoa huo na kuitikia wito wa wakazi wa mji huo.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Watumishi wa kikosi chetu wamepuliza dawa katika taasisi na ofisi za serikali, chini ya kufuata utaratibu maalum wa kupambana na virusi hivi, na kufuata maelekezo yaliyotolewa na taasisi za afya, aidha tuliunda kikosi cha dharura chenye jukumu la kutembelea nyumba za watu walioambukizwa virusi vya Korona na kuwawekea Oksijen, barakoa na vitakasa mikono.

Akafafanua kuwa: Tunatoa maelekezo ya afya na kugawa barakoa kwa wananchi, sambamba na kuwahimiza uvaaji wa barakoa na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, utendaji wetu unakubaliwa sana na wananchi, wanatoa pongezi nyingi kwa kikosi chetu.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kiliunda kamati ya kupambana na maambukizi mara tu baada ya kupatikana virusi vya Korona, kimesha puliza dawa sehemu nyingi hasa zenye wakazi wengi, na kinafanya kila kiwezalo katika kupambana na virusi hivi, ikiwa ni pamoja na kujenga sehemu maalum ya kuosha na kufanya shughuli zote za maziko kwa watu waliokufa kwa maradhi ya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: