Upasuaji wa aina yake.. kuondoa uvimbe na kupandikiza mfupa

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kuondoa uvimbe na kupandikiza mfupa kwenye taya ya chini ya mgonjwa mwenye umri wa miaka zaidi ya ishirini.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo Dokta Muammar Aaraji amesema kuwa: Jopo la madaktari wetu wamefanikiwa kuondoa uvimbe wote kwenye taya ya chini ya mgonjwa mwenye umri wa miaka (26) pamoja na kupandikiza mfupa wa bandia.

Akaongeza kuwa: Upasuaji huo umefanywa kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa sambamba na uwepo wa madaktari bingwa wenye weledi mkubwa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa wa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itowe ushindani mkubwa katika hospitali kubwa za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila baada ya muda fulani sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: