Kuanza kongamano la kimataifa awamu ya tatu likiwa na ushiriki wa kitaifa na kimatifa

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo mwezi (8 Shabani 1442h) sawa na tarehe (22 Machi 2021m), limeanza kongamano la kimataifa awamu ya tatu kuhusu udaktari na uhandisi, chini ya usimamizi wa chuo kikuu cha Alkafeel kikishirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel pamoja na chuo kikuu cha Malezia (UKM) ndani ya ukumbi wa Shekh Nasru-Dini Tusi katika kitivo cha udaktari wa meno, limefanywa kwa mtandao kupitia jukwaa la (ZOOM) na kwa kuhudhuria, ambapo tahadhari zote za kujikinga na maambukizi zimezingatiwa.

Kongamano limefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Ustadh Qassim Jaburi, halafi ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukasikilizwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya uliosomwa kwaniaba yake na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Halafu ukafuata ujumbe wa chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya uliowasilishwa na rais wake Dokta Nurisi Dahani.

Baada ya hapo ikaonyeshwa filamu ya kukitambulisha chuo kikuu cha Alkafeel na harakati zake kielimu, na mafanikio ambayo kimesha pata tangu kuanzishwa kwake.

Kisha Dokta Muhammad Saidi Abdu-Zuhura akawasilisha mada yenye anuani isemayo: (Essentials Curriculum Design).

Ukawa ndio ufunguzi wa kuwasilisha mada balimbali katika kumbi tofauti za chuo, mihtasari ya mada mbalimbali zipatazo (341) kutoka kwa watafiti wa ndani na nje ya Iraq ziliyo chachujwa kutoka kwenye jumla ya mada (535) imewasiliswa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: