Kuanza kwa shughuli za vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti kwenye kongamano la kimataifa awamu ya tatu

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya leo mwezi (8 Shabani 1442h) sawa na tarehe (22 Machi 2021m), vimeanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti katika kongamano la kimataifa awamu ya tatu linalo husu fani ya udaktari na uhandisi, linalo simamiwa na chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel pamoja na chuo kikuu cha Malezia.

Kwa mujibu wa maelezo ya chuo kikuu cha Alkafeel Ustadh Nuris Dahani amesema: “Tunatarajia kongamano hili liwe kituo cha kubadilishana fikra na hazina ya elimu na maarifa kwa wanachuoni na watafiti, na lifungue milango mipya ya fikra zinye matokeo mazuri kwa jamii”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya mada zilizo omba kushiriki kwenye kongamano zilifika (535), baada ya mchujo zikapasishwa mada (341), miongoni mwa mataifa yanayo shiriki ni: (Marekani, Ulaya, Kanada, Urusi, Bilarusia, China, Pakistani, Mlezia, Australia, India, Iran, Misri na Moroko) bila kuisahau Iraq iliyo wasilishwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kupitia vyuo vikuu (29) kumi na tisa (19) vya serikali na kumi (10) binafsi”.

Akafafanua kuwa: “Baadhi ya wizara zimekuwa na ushiriki wa wazi, kama vile wizara ya (afya, teknolojia, mafuta na kilimo), mada zote zilizo kubaliwa zitaandikwa kwenye jarida”.

Akasema: “Vikao vya uwasilishaji wa mada vitafanyika ndani ya kumbi tano, watakao hudhuria watatakiwa kuzingatia kanuni zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na wale watakao shiriki kwa njia ya mtandao watatumia jukwaa la (ZOOM) kupitia link ifuatayo: https://alkafeel-edu-iq.zoom.us/my/iscku
:Passcode
Kafeel

Mada za kitafiti zipo katika mgawanyo ufuatao:

  • - (medical and dentistry) mada 45.
  • - (Pharmacy) mada 63.
  • - (Engineering & Sciences) mada 77.
  • - (Medical and Health Techniques) mada 178”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: