Watafiti kutoka vyuo vikuu 29 vya kitaifa na kimataifa wanashiriki katika vikao vya kongamano la chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo mwezi (9 Shabani 1442h) sawa na tarehe (23 Machi 2021m), vimeanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kongamano la kimataifa awamu ya tatu kuhusu udaktari na uhandisi, linalo simamiwa na chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel pamoja na chuo kikuu cha Malezia.

Dokta Nawaal Aaidi Almayali rais wa chuo kikuu cha Alkafeel amesema kuwa: “Mada za kitafiti zimewasilishwa leo kwa njia ya mahudurio ya mubashara na njia ya mtandao kupitia jukwa la (ZOOM), mihtasari ya mada hizo imewasilishwa na kundi la watafiti wa masomo ya udaktari na uhandisi, kutoka vyuo vikuu ishirini na tisa ndani na nje ya Iraq, mada hizo zimetolewa kupitia kumbi tofauti, na zimepata muitikio mkubwa sambamba na majadiliano makali wakati wa uwasilishwaji wake jambo hilo linaonyesha umakini wa washiriki wa kongamano”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa wageni wa siku ya pili ni watumishi wa wizara wanaohusika na masomo ya mtandao katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, chini ya usimamizi wa Dokta Aamir Salim Amiri, na wamehudhuria kwenye vikao tofauti, wameupongeza uongozi wa chuo kufanya kongamano la aina hii pamoja na mada zilizo wasilishwa, wakasisitiza kuwa kongamano limepata mafanikio makubwa”.

Tambua kuwa mada za kitafiti zimewasilishwa kupitia kumbi kuu tano za chuo, washiriki walio hudhuria wamezingatia kanuni zote za kujikinga na maambukizi, huku wengine wakishiriki kupitia mtandao wa (ZOOM), mada zilizo wasilishwa zinahusu mambo yafuatayo:

  • - (Medical and dentistry).
  • - (Pharmacy).
  • - (Engineering & Sciences).
  • - (Medical and Health Techniques).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: