Mkuu wa hospitali ya Alkafeel: Tutafanyia kazi mambo yaliyo ongelewa katika kongamano

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel amesisitiza kuwa: “Mada nyingi zilizo wasilishwa kwenye kongamano ni nzuri na tutajitahidi kuzifanyia kazi, pamoja na kualika watafiti wa mada hizo kwa ajili ya kutoa muongozo wa namna bora ya kuzifanyia kazi”.

Akaongeza: “Hospitali ya rufaa Alkafeel husaidia harakati za kielimu ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu, na kongamano hili ni moja ya harakati muhimu, tumeshuhudia idadi kubwa ya mada zaidi ya (500) zilizo wasilishwa, ambapo baada ya kuzihakiki na kuzichuja zikapasishwa mada (340)”.

Akaendelea kusema: “Hospitali imewasilisha mada inayo husu ugumba na inaweza kufanyiwa kazi, tumeonyesha ukubwa wa tatizo hilo, itachapishwa na kusambavya siku za mbele kwa faida zaidi za kielimu”.

Naye Dokta Karim Ghanimi mkuu wa kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel amesema kuwa: “Kuna umuhimu wa kufanya makongamano haya ya kielimu kwa ajili ya kutumikia jamii na kuendeleza nchi zetu, chuo kikuu cha Alkafeel kimeshafanya makongamano mengi na nadwa mbalimbali, na kongamano hili ni sehemu ya kusambaza uzowefu wa kielimu kwenye mipaka ya dunia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: