Rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed amesema: Mada zinazo wasilishwa katika kongamano hili zitaandikwa kwenye magazeti ya kimataifa

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Muayyad Imrani Alghazali amesema: “Mada zinazo wasilishwa kwenye kongamano hili la kimataifa awamu ya tatu kuhusu udaktari na uhandisi, zitaandikwa kwenye magazeti ya kimataifa”.

Akaongeza kuwa: “Tunathamini sana mada zinazo wasilishwa kwetu na ndio maana tunakuwa makini kuuliza faida ya mada kwani tunalenga kutumikia jamii”.

Naye Ustadh Ali Jaasim Ramadhani Al-Aamiriy mkuu wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Alkafeel amesema kuwa: “Tumepokea mada (284) za masomo ya sayansi na uhandisi, baada ya kuzihakiki na kuzichuja zikapasishwa mada (208), zote zitaandikwa kwenye ukumbi wa maelezo na tayali zimejadiliwa katika kongamano hili kupitia vikao (12)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: