Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiismalamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya kongamano la usomaji wa mashairi katika kusherehekea kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) walio zaliwa ndani ya mwezi huu mtukufu wa Shabani, (Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad pamoja na Imamu wa zama Almahadi msubiriwa –a.f-).
Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Kongamano limefanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom), washairi walioshiriki wametoka mikoa ya (Najafu, Baabil, Basra), kaswida zao zilikuwa zinahusu kuwapenda Ahlulbait (a.s) na utukufu wao, hii ni moja ya harakati ambazo hufanywa na Maahadi”.
Akasema: “Watu wanatakiwa kufundisha utamaduni wa kusoma Quráni na kuwapenda Ahlulbat (a.s) hususan katika mwezi huu mtukufu wa Shabani”.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inalenga kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, pamoja na elimu ya usomaji wa Quráni tukufu, sambamba na kutengeneza kizazi cha wanawake wanaofanyia kazi mafundisho ya Quráni na sunna na wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu kuhusu Quráni tukufu.