Uwanja wa Saaqi umefika katika hatua ya mwisho

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa kazi ya kupanua uwanja wa Saaqi imefika katika hatua ya mwisho na kilicho baki ni umaliziaji tu, sehemu hiyo itajumuishwa na sehemu zingine za uwanja huo, na itasaidia katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru na mawakibu wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, na kupunguza msongamano ambao hutokea kwenye barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani sehemu iliyo ongezwa itasaidia misafara ya mazuwaru kupita kwa urahisi, sehemu iliyo ongezwa inaukubwa wa (mt 10) zilizo gawanywa pande mbili za barabara.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa kwenye mtandao wa Alkafeel na msimamizi wa kazi hiyo Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, akaongeza: Kilicho baki ni kuweka marumaru sehemu ya mwisho (nayo ni sehemu ndogo sana ukilinganisha na sehemu iliyokamilika) ipo upande wa kulia wa barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na nakshi zitakazo wekwa upande wa soko”.

Akabainisha kuwa: “Eneo lililo ongezwa linaukubwa wa mita (1610), limejengwa ujenzi wa chini kama vile (umeme, njia, mfumo wa mawasiliano, kamera, na mfumo wa maji safi kwa kunywa), pamoja na kuweka lami baadhi ya sehemu na uwanja huo unaungana na barabara”.

Kumbuka kuwa mradi huu ni kwa ajili ya kupunguza msongamano wa watu ambao hutokea eneo hilo na kuongeza idadi ya mazuwaru wanaotumia barabara hiyo hususa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambazo huwa na msongamano mkubwa, ambapo huathiri utendaji wao wa ibada na ziara kutokana na kushindwa kuingia ndani ya Ataba tukufu, kwani sehemu hii ni moja ya pande muhimu zinazo tumiwa na mazuwaru wengi kutokana na utukufu wa mlango huu katika nyoyo za watu wanaokuja kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: