Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kumsaidia kujifungua msichana kutoka Bagdad mwenye tatizo la kufeli moyo, hospitali nyingi zilikataa kumpokea kwa kuhofia maisha yake.
Daktari bingwa wa wanawake na ukunga Dokta Azhari Abdu Faliih amesema: “Mgonjwa alikuwa na ujauzito wa miezi tisa, anatatizo la kufeli moyo na uchache wa damu, alikuwa amesha fanyiwa upasuaji mara tatu, na alikuwa chini ya uangalizi maalum baada ya upasuaji”.
Akafafanua kuwa: “Uwezo wa hospitali ya Alkafeel na vifaa-tiba vya kisasa ilivyo navyo vinamchango mkubwa wa kupokea mgonjwa wa aina hii, kama sio kuwepo kwa vifaa hivyo ingekuwa vigumu kumpokea”.
Akaongeza kuwa: “Baada ya kumfanyia vipimo tumefanya upasuaji kwa mafanikio, baada ya saa (24) tangu kufanyiwa upasuaji huo mgonjwa ameruhusiwa pamoja na mwanae wote wakiwa na afya nzuri”.
Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma kwa kutumia vifaa-tiba bora na vya kisasa zaidi, chini ya madaktari bingwa wa kitaifa na kimataifa jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimaiafa duniani.
Kumbuka kuwa hospitali ya kimataifa Alkafeel hualika madaktari bingwa walio bobea katika maradhi tofauti kila baada ya muda fulani, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali mbalimbali za maradhi yao.