Mwezi kumi na moja Shabani alizaliwa mtu anayefanana zaidi na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Mwezi kumi na moja Shabani tunakumbuka kuzaliwa kwa Ali Akbaru (a.s), mjikuu wa kiongozi wa waumini na mbora wa wanawake wa ulimwenguni na mtoto wa bwana wa mashahidi (a.s), alizaliwa mwaka wa (33) hijiriyya, riwaya zinasema kuwa alizaliwa katika mji wa Madina.

Alikuwa kinara mtukufu wa bani Hashim aliyefundisha uislamu wa kweli na akaonyesha namna ya kujitolea, aidha ni mmoja wa nyota za Karbala, aliuwawa katika vita ya Karbala akimtetea bwana wa mashahidi (a.s).

Ali Akbaru (a.s) anasifika kwa sura nzuri, anapendeza ukimwangalia, alikuwa na mwenendo mzuri, ni fahari kwake kuwa alifanana sana na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), katika uongeaji, tabia na maumbile, babu yeke Ali bun Abu Twalib (a.s) alikuwa anazungumza sana hadithi zinazo onyesha kufungamana kwake na elimu pamoja na ukamilifu toka akiwa mdogo.

Mzazi wake Imamu Hussein (a.s) alisema kauli mashuhuri katika uwanja wa Karbala: (Ewe Mola shuhudia, ametoka kwao kijana anayefanana zaidi umbo, tabia, kuongea na Mtume wako, tulikuwa tunapo mkumbuka Mtume tunamuangalia kijana huyu).

Hussein (a.s) alikuwa anaangalia uso wa Ali Akbaru na kuuona sawa na uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kila kitu alichokuwa akikiona kwake kilikuwa kinamkumbusha babu yake, kutembea kwake, kukaa kwake, kutabasamu kwake, adabu yake, furaha yake, kuchukia kwake, hakika alifanana na Mtume kwa kila kitu.

Ushujaa wake:

Imepokewa kuwa pindi alipo ondoka Imamu Hussein katika nyumba za bani Muqaatil, Imamu Hussein (a.s) alisema: Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, -mpokezi anasema- akasema hivyo mara mbili au mara tatu. Mwanae Ali akamgeukia na akasema: Ewe baba kwanini umesema maneno hayo? Akasema: ewe mwanangu mimi nimepata bishara kuwa msafara huu unatembea na kifo kinawafuata, nikatambua kuwa nafsi zetu zinakaribia kutoka, akasema: Ewe baba hajawahi kukuonyesha Mwenyezi Mungu jambo baya, hivi hatuko katika haki? Akasema: tupo kwenye haki. Akasema: Ewe baba tusijali tutakufa tukiwa katika haki, akasema: Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Msimamo wake siku ya kumi:

Imepokewa kuwa Imamu Hussein (a.s) siku ya kumi alibaki na watu wa nyumbani kwake pamoja na wale wa karibu yake, Ali akamfuata baba yake na kumuomba ruhusa ya kwenda kupigana, akaruhusiwa, Imamu akamuangalia kwa huruma na akalia kisha akasema: Ewe Mola shuhudia ametoka kwao kijana anayefanana zaidi na Mtume wako (s.a.w.w), tulikuwa tunapomkumbuka tunamuangalia kijana huyu..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: