Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Dini, imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Ali Akbaru, mtu anayefanana zaidi na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), aliye zaliwa siku kama ya leo mwezi (11 Shabani), wameratibu mihadhara ya kidini inayo tolewa ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mhadhara umetolewa na Shekh Muhsin Asadi, amezungumza mambo mengi kuhusu historia ya mtukufu huyu ambaye jina lake limeandikwa kwa herufi za nuru katika vitabu vya historia, amebainisha utukufu wa Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s) na nafasi yake mbele ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), utukufu wake unaonekana wazi pale alipotoka kwenda kupigana siku ya Ashura (mwezi kumi Muharam), alikuwa Hashimiyya wa kwanza kupigana baada ya kuruhusiwa na baba yake Imamu Hussein (a.s), Imamu (a.s) alimuangalia kwa jicho la huruma kisha akalia halafu akaangalia mbinguni na kusema: (Ewe Mola shuhudia hawa watu, ametoka kwao kijana anayefanana zaidi na Mtume wako umbo, tabia na kuongea, tulikua tunapo mkumbuka Mtume tunamuangalia kijana huyu, ewe Mola wanyime baraka za ardhi na uwafarakishe na kuwagawanya, wafanye wawe makundi makundi wala usiwaridhie milele, wametwita kutunusuru kisha wamegeuza siraha kwetu kutuuwa).
Hali kadhalika ameongea kuhusu hadhi ya Ali Akbaru (a.s) mbele ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), katika ziara tukufu tunaona Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Kwa haki ya baba wewe na mama kwa aliyechinjwa na kuuwawa bila kosa).