Moja ya hatua za kukarabati pambo la malalo ya Abulfadhil Abbasi ipo katika hatua za mwisho

Maoni katika picha
Kazi inayo endelea katika pambo la malalo ya Apulfadhil Abbasi (a.s) ipo katika hatua za mwisho, kazi hizo ni pamoja na uwekaji wa marumaru kwenye ukuta wake pamoja na vyumba vya ofisi, na kwenye ukumbi wa haram hadi uwanja wa haram tukufu upande wa kushoto kwa ndani, nayo ni sehemu ya pili katika kazi hii, baada ya kumaliza sehemu kubwa ya upande wa kulia, kwenye eneo linalo kadiriwa kuwa nusu ya uwanja huo yenye ukubwa wa mita (500).

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesema kuwa: “Tunafanya kazi saa (14) kwa siku kwa ajili ya kumaliza haraka hatua muhimu ambayo ni kukarabati ukuta na kuweka marumaru kabla ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani”.

Akaongeza kuwa: “Kazi zilizo tangulia zilikua ni maandalizi ya uwekaji wa marumaru, ilikuwa ni kuondoa marumaru zilizokuwa zimeharibika na kuondoa tabaka la smenti (saruji) hadi kufika kwenye tabaka la udongo, kisha kuweka udongo (kifusi) maalum kitakacho saidia kuimarisha ukuta wa haram na nguzo za sega la pambo, pamoja na kuongeza uimara zaidi wa sakafu, kisha watumishi wa shirika la ujenzi wakaanza kazi ya kuweka tabaka la smenti (saruji) baada ya hapo wanaweka marumaru za aina ya (Malti-Oksi), aina hiyo pia ndio iliyowekwa katika uwanja wa haram tukufu na korido zake”.

Akaongeza kuwa: “Kazi hiyo imehusisha pia kuweka marumaru kwenye vyumba vya watumishi vilivyopo sehemu hiyo, kazi imefika hatua nzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: