Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imezindua semina tatu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imezindua semina tatu za ufundishaji wa hukumu za usomaji wa Quráni tukufu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Maahadi inapokea wanafunzi wa kila umri, hivi sasa imezingua semina tatu za makundi ya umri tofauti”.

Akafafanua kuwa: “Kuna kundi la (Kaadhimul-Ghaidh) ya watu wenye umri wa miaka (14 – 17), na kundi la (Aáraaf) la wasichana wa chuo, na kundi la (Safinatu-Najaa) kwa wenye umri mkubwa, hiyo ni kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi na kulinda utukufu wa Quráni”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inalenga kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, ikiwemo maarifa ya Quráni, na kutengeneza kizazi cha wanawake wanaofanyia kazi mafundisho ya Quráni na wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za masomo ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: