Waziri wa afya anaangalia maandalizi ya Atabatu Abbasiyya katika ziara ya Shaábaniyya

Maoni katika picha
Waziri wa afya Sayyid Hassan Tamimi, Alasiri ya Ijumaa mwezi (12 Shabani 1442h) sawa na tarehe (26 Machi 2021m), ametembelea Atabatu Abbasiyya akiwa na bwana afya wa mkoa wa Karbala kuangalia mazingira ya afya yaliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kupokea ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.

Baada ya kufanya ibada ya ziara na kusoma dua Mheshimiwa waziri amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar, aliye eleza mkakati wa afya ulioandaliwa na Atabatu Abbasiyya katika ziara ya Shaábaniyya, pamoja na kueleza hatua zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kusaidia taasisi za afya zilizo chini ya serikali katika vita ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kwenye mikoa tofauti, na misafara ya kupuliza dawa, ambayo bado inaendelea, pamoja na mambo mengine mengi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: