Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Shaábaniyya

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kisheria kwa mawakibu zitakazo shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani, maandalizi hayo ni moja ya mambo muhimu ambayo hufanywa na kitengo hicho kwa kushirikiana na idara ya askari wa Karbala, hairuhusiwi kushiriki maukibu yeyote bila kupasishwa na kupewa utambulisho maalum na kitengo hiki.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Niímah Salmaan, akaongeza kuwa: “Ziara ya mwezi kumi na tano Shabani ni miongoni mwa ziara zinazo huduriwa na mamilioni ya watu katika ardhi tukufu ya Karbala, na hushiriki idadi kubwa ya mawakibu za kutoa huduma kwa mazuwaru, nazo ni mawakibu maalum kwa ziara hii, pia kuna mawakibu maalum za ziara ya Arubainiyya na ziara ya Ashura, pamoja na mawakibu ambazo hutoa huduma kila siku, hivyo tangu mwanzo wa mwezi huu tunapokea viongozi wa mawakibu kwa ajili ya kuwapa vitambulisho maalum vya mawakibu zao, hilo ni jambo muhimu sana kiusalama na kitaratibu katika kuratibu kazi za mawakibu kwa ujumla, shughuli hiyo hufanywa kwa kushirikiana na mamlaka husika katika askari wa Karbala, majina ya mawakibu zote yameandikwa katika ukurasa maalum wa kitengo cha mawakibu, baada ya hapo hupewa kibali cha kuruhusiwa kutoa huduma”.

Akaongeza kuwa: “Ziara ya mwaka huu itakua ya aina yake kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, kwa hiyo tumeandaa utaratibu unao endana na mazingira hayo, mawakibu za kutoa huduma zitakuwa mbali na malalo mawiti takatifu, na tumesisitiza watumishi wa mawakibu wazingatie maelekezo yote ya kujikinga na maambukizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: