Maahadi ya Quráni tukufu anafanya semina kwa njia ya mtandao yenye ushiriki wa kimataifa

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya semina ya Quráni kwa njia ya mtandao awamu ya tatu katika usomaji wa tajwidi, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (200) kutoka nchi tano na mikoa kumi na nne ya Iraq, masomo yanatolewa kwa njia ya mtandao kupitia majukwaa ya mawasiliano ya kijamii.

Semina hii inaendeshwa katika kipindi ambacho taifa lipo katika tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, semina hiyo inafanywa chini ya usimamizi wa msomaji Ahmadi Zaamiliy ambaye anawapa washiriki masomo ya (usomaji sahihi na hukumu za usomaji) kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Tambua kuwa tawi la Maahadi limeweka sharti la umri wa kushiriki kuwa ni miaka (15 – 45) na muda wa semina ni zaidi ya siku (45) kwa kusoma saa moja na nusu kila siku, na kila wiki itakuwa na siku tatu za masomo.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Quráni ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha Quráni na kuandaa jamii inayo fanyia kazi mafundisho ya Quráni na yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika mambo tofauti yanayo husu Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: