Muonekano wa mapambo ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f).

Maoni katika picha
Kumbukumbu za mazazi katika mwezi wa Shabani zimeanza tangu mwezi tatu Shabani, kwa kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s), na sasa tunasherehekea kuzaliwa kwa Imamu wa kumi na mbili, hoja wa Mwenyezi Mungu mtukufu wa watu wote, Hujjat bun Hassan Almahadiy Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) ambae tarehe yake ya kuzaliwa kwake inasadifu siku ya Jumatatu mwezi (15 Shabani 1442h).

Kutokana na kumbukumbu hii tukufu kuta na korido za Atabatu Abbasiyya tukufu zimewekwa mapambo, na kufungwa vitambaa vilivyo andikwa maneno mazuri ya pongezi, na zimewashwa taa za randi maalum ndani ya uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya tukio hili, pamoja na kuweka chupa za mauwa na miti ya mapambo kwenye milango ya haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: