Andikisha jina lako miongoni mwa mazuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umetangaza kuwa utafanya ibada ya ziara maalum ya mwezi kumi na tano Shabani ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa niaba ya kila atakaeshindwa kuja kufanya ziara kutokana na mazingira ya sasa ya janga la virusi vya Korona au kwa sababu nyingine, kupitia dirisha la ziara kwa niaba katika link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara

Ziara hiyo itafanywa na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao ni masayyid kwa niaba ya waumini wa kiume na wakike waliopo kila sehemu ya dunia, katika tukio hili la kuadhimisha kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.f) na ziara maalum ya mwezi kumi na tano Shabani usiku na mchana, ibada hiyo ni pamoja na kusoma ziara kuswali na kusoma dua mbele ya malalo takatifu.

Kumbuka kuwa kuna riwaya nyingi zinazo eleza kuhusu utukufu wa kufanya ziara mwezi kumi na tano Shabani, tena zimepokewa kwa vyanzo vingi vinavyo aminika, kutoka kwa Imamu Zainul-Aabidina na Imamu Swadiq (a.s) wanasema: (Anaetaka kuwapa mkono mitume laki moja na elfu ishirini na nne alizuru kaburi la Abu Abdillahi Hussein bun Ali (a.s) mwezi kumi na tano Shabani, hakika roho za Mitume (a.s) huomba ruhusa kwa Mwenyezi Mungu ya kuja kumzuru, naye huwaruhusu. Amefaulu atakaewapa mkono na Mitume hao wakampa mkono, wakiwemo mitume watukufu zaidi watano, ambao ni Nuhu, Ibrahim, Mussa, Issa na Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: