Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya leo siku ya Jumapili (14 Shabani 1442h) sawa na tarehe (28 Machi 2021m), imezindua nakala ya mwisho ya kitabu cha fatwa kifaya ya kujilinda yenye juzuu (62), sambamba na kuadhimisha mwaka wa saba tangu kutolewa kwa fatwa hiyo, iliyo linda ardhi ya Iraq na maeneo yake matakatifu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu pamoja na naibu wake na wajumbe wa kamati kuu.
Tambua kuwa kitabu hiki ni cha kwanza kwa ukubwa miongoni mwa vitabu vilivyo andika kuhusu fatwa ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, iliyo itikiwa na raia wa Iraq kwa kujiunga katika vikosi vya wapiganaji kupambana na magaidi wa Daesh.