Katibu mkuu wa Ataba tukufu: Tumejitahidi kuonyesha picha ya mashujaa wa fatwa kwa vizazi vijavyo.

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar, amesisitiza kuwa wamelipa umuhimu swala la kuonyesha picha ya mashujaa wa fatwa ya jihadi kifaya kwa vizazi vijavyo, kizazi baada ya kizazi, ukizingatia kuwa matukio hayo yameandikwa kutoka kwenye uwanja halisi wa vita.

Akaongeza: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda kimeandikwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kitabu hiki kina juzuu (62), kimeandika ushujaa wa wapiganaji walio itikia wito wa fatwa ya kujilinda na wakajitolea kila kitu kwa ajili ya kulinda Iraq na maeneo matakatifu”.

Tambua kuwa kitabu hiki ni cha kwanza kwa ukubwa katika vitabu vilivyo andika kuhusu fatwa ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, na kuitikiwa kwa wingi na raia wa Iraq walio kwenda kujiunga katika vikosi vya wapiganaji, kwa ajili ya kulinda ardhi na heshima pamoja na kuitikia wito wa Marjaa wao wa kupambana na magaidi wa Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: