Kuzaliwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.s)

Maoni katika picha
Umma wa kiislamu upo katika maadhimisho muhimu sana, maadhimisho ya kukumbuka kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.f), naye ni Imamu wa kumi na mbili katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s) walio bashiriwa na Mtume (s.a.w.w) pale alipo sema: (Baada yangu kutakuja makhalifa kumi na mbili wote wanatokana na makuraishi), nao wanatokana na kizazi kitakatifu cha Fatuma Zaharaa na ni katika wajukuu wa Imamu Hussein Shahidi (a.s).

Vitabu vya historia pamoja na riwaya zimethibitisha kuzaliwa kwa Imamu Muhammad msubiriwa (a.f), hakika ilikuwa ni kawaida ya bibi Hakimah (Mtoto wa Imamu Jawaad na Ammi yake Imamu Hassan Askariy -a.s-), kila anapo mtembelea mtoto wa kaka yake anamuomba Mwenyezi Mungu amruzuku mtoto wa kiume, anasema: Niliingia kwake siku moja nikasema kama ninavyo semaga na nikaomba kama ninavyo ombaga, akasema: Ewe Shangazi hakika unayeniombea Mwenyezi Mungu aniruzuku atazaliwa usiku huu, ewe shangazi leo lala hapa hakika atazaliwa mtoto mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, bibi Hakimah akasema: Atazaliwa na nani ewe bwana wangu, sioni athari ya ujauzito kwa Narjisi, akasema: kwa Narjisi hakuna mwingine.

Akasema: Nikaingia kwa Narjisi nikamuangalia mgongoni sikuona athari ya ujauzito, nikarudi kwake nikamuambia nilicho fanya, akatabasamu kisha akaniambia: Ukifika wakati wa Alfajiri itadhihiri kwako athari ya mimba, kwa sababu mfano wake ni sawa na mama wa Mussa mimba yake haikudhihiri, hakuna yeyote aliyemtambua kuwa ni mjamzito hadi wakati wa kujifungua, kwa sababu Firauni alikuwa anapasua matumbo ya wanawake wajawazito kwa ajili ya kumtafuta Mussa na huyu ni sawa na Mussa -a.s- (atamaliza utawala wa matwaghuti).

Nikaendelea kumuangalia hadi wakati wa Alfajiri huku yeye akiwa amelala, ilipo fika Alfajiri akapatwa na uchungu, nikamsikia Imamu anasema: Msomee (Innaa Anzalnaahu fii lailatil-Qadri) nikamsomea, akaniambia imedhihiri kama alivyo kuambia Imamu, nikaendelea kumsomea kama nilivyo amrishwa, akanipokea mtoto aliyekuwa tumboni, akawa anasoma kama mimi nilivokua nasoma, halafu akanitolea salam.

Bibi Hakimah anasema: Nikashangazwa na nilicho sikia, Imamu Askariy (a.s) akaniambia: Usishangae amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu hutuzungumzisha kwa hekima tukiwa wadogo na hutufanya hoja tunapokuwa wakubwa, kabla hajamaliza kuongea bi Narjisi akatoweka ikawa kama baina yake na mimi kuna pazia, nikaenda upande wa Imamu Askariy (a.s) nikiwa naita, akasema: Ewe shangazi yangu rudi utamkuta palepale alipokua.

Akasema: Nikarudi baada ya muda mfupi pazia ikaondoka baina yangu na yeye, nikamuona akiwa na mwanga ulioumiza macho yangu, mara nikamuona mtoto akiwa kasujudu na ameinua mikono yake juu huku anasema: (Nashuhudia hakuna Mola ispokua Allah mmoja asiyekua na mshirika na babu yangu ni mtume wa Mwenyezi Mungu na baba yangu ni kiongozi wa waumini… halafu akataja Imamu mmoja baada ya mwingine hadi akafika kwake.

Akasema (a.s): Ewe Mola kamilisha ahadi yangu, ukamilishe amri yangu, uthabitishe miguu yangu, ujaze ardhi uadilifu na haki kupitia mimi…
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: