Ziara kwa mbali katika malalo ya Abulfadhil Abbasi na kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetangaza kuanzisha mfumo unaotoa fursa ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) ukiwa mbali na kutembelea Ataba yake takatifu, kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel (mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu), katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu wa zama Hujjat Almuntadhir (a.f), kwa ajili ya kumuwezesha kila aliyeshindwa kuja kufanya ziara kutokana na janga la virusi vya Korona.

Mkuu wa kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel Ustadh Bashiri Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mfumo huu umetengenezwa kwa kushirikiana na idara ya teknolojia pamoja na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umeanzishwa kutokana na kuwepo wa janga la virusi vya Korona, linalo sababisha raia wengi wa ndani na nje ya Iraq kushindwa kuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Program hii inatoa fursa kwa mtumiaji wa kompyuta au simu kufanya ziara kwa kutumia faili la sauti lililo andaliwa maalum kwa ajili ya ziara, na kutembea ndani ya korido za Atabatu Abbasiyya na haram takatifu na sehemu yake ya juu, huduma hiyo imepewa ukurasa maalum katika mtandao wa Alkafeel, hii ni hatua ya kwanza zitafuata hatua zingine, zitakazo husisha sehemu zingine za ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya”.

Mpiga picha wa program hii bwana Saamir Husseini kutoka kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel amesema kuwa: “Mfumo huu (banurama) unahusisha picha zaidi ya (250) zenye ubora mkubwa, kila picha inaonyesha sehemu maalum ya Ataba tukufu, zimewekwa kwa mfumo wa daraja (360) ili kumpa fursa ya kuangalia kwa urahisi mtu anayefanya ziara, picha zote zilizo pigwa hivi sasa ni za kisasa zaidi zinaendana na mfumo huu, hii ni mara ya kwanza tunatarajia kuboresha zaidi ziku zijazo, na kuongeza sehemu zingine za ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: