Haya ndio yaliyofanywa na idara ya usimamizi wa Haram katika ziara ya Shaábaniyya

Maoni katika picha
Idara ya usimamizi wa Haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya kazi kubwa ya kupokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara tukufu ya Shaábaniyya, kupitia watumishi wake wote kila mmoja katika jukumu alilo pangiwa.

Tumeongea na kiongozi wa idara hiyo bwana Nazaar Ghina Khaliil kuhusu swala hilo amesema kuwa: “Watumishi wetu walianza kutekeleza majukumu yao mbalimbali katika ziara ya Shaábaniyya, miongoni mwa majukumu hayo ni kupangilia matembezi ya mazuwaru wanapo ingia na kutoka ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya kuondoa msongamano katika matembezi yao”.

Akaongeza kuwa: “Tuliandaa sehemu maalum za kuswalia na kusoma dua ndani ya haram tukufu”. Akaendelea kusema: “Tuliandaa watumishi maalum kwa ajili ya kusaidia watu wenye umri mkubwa na watu wenye ulemavu wakati wa kufanya kwao ziara, pia kunawatumishi maalum waliopewa mafunzo ya utoaji wa huduma za kwanza za afya kwa kushirikiana na idara ya madaktari, kwa ajili ya kupambana na tatizo lolote la kiafya kama likitokea Allah atuepushie”.

Kuhusu utaratibu wa kujilinda na maambukizi amesema kuwa: “Kazi ya kupuliza dawa imefanyika wakati wote siku nzima, pamoja na utumiaji wa vitakasa mikono na uvaaji wa barakoa kabla ya kuingia katika haram tukufu”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi tote tumefanya kwa kushirikiana na watu wa kujitolea waliokuja kutoka mikoa tofauti kuwahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: