Zaidi ya maukibu (600) zimetoa huduma katika ziara ya Shaábaniyya

Maoni katika picha
Kitendo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimesema kuwa, maukibu zilizo shiriki kutoa huduma katika ziara ya mwezi kumi na tano Shabani mwaka huu na zilizo sajiliwa rasmi ni (620) zikiwemo tatu kutoka nje ya Iraq.

Hayo yamesemwa na rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Niímah Salmaan, akaongeza kuwa: “Watumishi wa kitengo hiki walifanya kazi ya kuhakiki maukibu hizo na kutoa vibali kwa kushirikiana na polisi wa Karbala, sambamba na kuwapa baadhi ya watumishi wake jukumu la kusimamia utekelezaji wa kanuni za afya, ikiwa ni pamoja na umbali kati ya mtu na mtu ili kulinda usalama wa mazuwaru”.

Akafafanua kuwa: “Mawakibu zilizoshiriki kutoa huduma ziliwekwa kama ilivyo pangwa, vituo vyao vilijengwa kando ya barabara zinazo elekea katika Ataba mbili tukufu mbali na Ataba hizo kwa ajili ya kuepusha msongamano, mawakibu hizo zimegawa chakula na vinywaji pamoja na kuandaa sehemu za kulala na huduma zingine, zikiwemo tiba na vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: