Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa ratiba yake ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani imefanikiwa

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa ratiba yake ya ulinzi, utoaji wa huduma na utekelezaji wa kanuzi za afya iliyo andaa kwa ajili ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani, kila kitu kimefanyika vizuri bila kikwazo chochote, na tumefikia malengo tuliyo jiwekea ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ziara kwa amani na utulivu.

Mafanikio haya yanatokana na juhudi za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ushirikiano wa mazuwaru watukufu pamoja na kuwa na vitendea kazi stahiki kwa kila kitengo, japokuwa tupo katika mazingira ya uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona, idara ya afya iliweka vipaombele vyake na kutengeneza mazingira ya kulinda afya za mazuwaru na watoa huduma, sambamba na kufanyia kazi maelekezo ya wizara ya afya.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa shukrani kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na idara za kutoa huduma na mawakibu Husseiniyya kwa kazi kubwa waliyo fanya, ambayo imefanikisha kufanyika kwa ziara hii tukufu kwa amani na usalama bila usumbufu wowote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: