Zowezi kubwa la usafi lashuhudiwa katika uwanja wa katikati ya haram mbiti tukufu

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kinaendesha zowezi kubwa la kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili na sehemu iliyo pauliwa pamoja na barabara zinazo elekea kwenye uwanja huo na maeneo yote yanayo zunguka sehemu hiyo, baada ya kuisha ziara ya mwezi kumi na tano Shabani, kazi hiyo inahitimisha usafi uliokuwa unafanywa wakati wa ziara kwa kutumia watumishi na vifaa vyake.

Rais wa kitengo hicho Ustadh Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu hufanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru katika kila msimu wa ziara, husaidia kuweka mazingira mazuri ya kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu, pamoja na mazingira magumu ya sasa yanayo sababishwa na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, miongoni mwa kazi ambazo huwa tunafanya ni kusafisha uwanja wote wa katikati ya haram mbili tukufu na sehemu zinazo zunguka uwanja huo wakati wa ziara na baada yake, sambamba na kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wote wa kitengo chetu wameshiriki katika kazi hii, wamefanya usafi kwa kutumia vifaa vya kitengo, wamemaliza kusafisha haraka sehemu tulizo taja, wameondoa uchafu wote kwenye barabara zinazo zunguka uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, hadi kwenye maeneo ya mji wa zamani”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kazi kubwa wakati wa ziara ya Shaábaniyya ya kuwahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) waliokuja kwa wingi katika mji wa Karbala na kuingia kwenye uwanja mtukufu wa katikati ya haram mbili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: