Kujadili mchoro wa mwisho katika mradi wa ujenzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa mikutano katika kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimefanyika kikao cha kujadili mchoro wa mwisho wa mradi wa jengo jipya la chuo kikuu cha Al-Ameed, unao tarajiwa kutekelezwa hivi karibuni.

Kikao hicho kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Muayyad Ghazali pamoja na msaidizi wake, na kiongozi wa idara ya usanifu katika kitengo cha miradi ya kihandisi, Mhandisi Muhammad Naswifu, aliyetoa maelezo kuhusu mchoro huo, ulio andaliwa baada ya upembuzi yakinifu ulio pelekea kuandaliwa mchoro huo utakao jadiliwa tena siku chache zijazo na kufanya maamuzi ya mwisho.

Wahudhuriaji wametoa maoni na mapendekezo yao kuhusu mchoro huo, ni matarajio yetu kikao kijacho tutafikia maamuzi ya mwisho.

Kumbuka kuwa mchoro unao jadiliwa unamajengo saba ya kitivo cha udaktari wa meno, uuguzi, na vitivo viwili vingine, pamoja na maabara yake, na maabara kuu, jengo la utawala na jengo la maktaba kuu, pamoja na sehemu ya bustani na sehemu za kupumzika, eneo lote jumla linaukubwa wa dunam (40) ambazo ni sawa na (heka ishirini), muda uliopangwa katika ujenzi wa mradi huo ni miaka mitatu, na chuo hicho kinatarajiwa kuwa kitovu cha elimu katika mkoa wa Karbala, chuo hicho kitakidhi vigezo wa kimataifa na vya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na kitakuwa na mazingira bora kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: