Kitengo cha maendeleo endelevu kimetoa mhadara kwa watumishi wa kituo cha turathi za Hilla, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, wamefundisha namna ya kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii katika maendeleo ya teknolojia.
Mhadhiri bwana Twaha Fadhili amesema: “Tulikua katika wenyeji wa kituo cha turathi za Hilla ikiwa ni sehemu ya harakati za kitengo cha maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kuwajengea watumishi uwezo wa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.
Akaongeza: “Tumeongea kuhusu njia ya uongeaji inayo pendwa na vijana wa kiislamu, inayoweza kuwasaidia kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) katika maisha yao”.
Mhadhiri bwana Muhammad Yaasiri amesema kuwa: “Watumishi walikua wanajua majukumu yao, kwani wanafanya kazi chini ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mhadhara ulikuwa na matunda mazuri”.
Mkuu wa kituo cha turathi za Hilla Sheikh Swadiq Khawilidi amepongeza kazi kubwa inayo fanywa katika swala hili la uelekezaji, linalo jenga uwelewa kwa watumiaji wote wa mitandao ya mawasiliano ya kijamii hasa vijana.