Daru-Makhtutwaat ya Iraq: inafanya juhudi ya kukuza ushirikiano na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya turathi za nakala-kale

Maoni katika picha
Mkuu wa Daru-Makhtutwaat za Iraq Dokta Ahmadi Alyawi amesema: “Sisi tunataka kuimarisha ushirikiano na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sekta ya turathi za nakala-kale na kusaidia utunzaji wake na kuzionyesha zikiwa katika muonekano mzuri, kwa faida ya watafiti wa mambo ya turathi, pamoja na kubadilishana uzowefu baina yetu katika sekta hii”.

Yamesemwa hayo katika ziara iliyofanywa na wajumbe wa kituo cha ukarabati wa nakala-kale pamoja na kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi ya Ataba tukufu, wamejadili mambo mengi ikiwa ni pamoja na kufanya semina za mambo ya faharasi na upigaji picha, na kuangalia ushiriki wa vituo vya nakala-kale katika harakati zinazo fanywa na Daru, ikiwa ni pamoja na harakati ya (siku ya nakala-kale za kiarabu) ambayo hufanywa ndani ya kumbi za makumbusho ya taifa la Iraq mwezi wa nne, huhudhuriwa na vituo vingi pamoja na taasisi za turathi, hapo huonyeshwa aina tofauti za nakala-kale, wamejadili jinsi ya kuongeza ushirikiano katika sekta hiyo, kutokana na umuhimu wake katika historia ya Iraq.

Mwisho wa kikao hicho Alyawi akawashukuru wajumbe kwa kuja kwao na utayari wao wakushirikiana na Daru, akaomba vokao kama hivi viendelee kufanyika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: