Kutangaza majina ya walioshinda kwenye shindano la kuhifadhi na kusoma khutuba ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya walioshinda kwenye shindano lililofanywa kwa njia ya mtandao na kuhusisha wanawake, la kuhifadhi na kusoma khuruba ya bibi Zainabu (a.s) aliyotoa mbele ya Yazidi (laana iwe juu yake), jumla ya washiriki walikua (288) kutoka ndani na nje ya Iraq, shindano hilo limefanywa sambamba na kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).

Hakika shindano hilo limepata muitikio mkubwa “Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa, tuliunda kamati ya kuchuja majibu sahihi na ikatuletea washindi (69)”.

Akaongeza kuwa: “Washindi watatu wa kwanza tumewapa zawadi ya hela na walio baki tumewapa zawadi zingine, hafla ya kutoa zawadi imefanywa ndani ya sardabu ya Imamu Ali Alhaadi (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akamaliza kwa kusema: “Shindano hili wameshiriki wanawake wenye umri tofauti, ilikuwa fursa nzuri ya kutambua malengo ya khutuba na athari zake”.

Kumbuka kuwa shindano hili lilikua sehemu ya kukumbuka kifo cha bibi Zainabu (a.s), aliye fariki mwezi kumi na tano Rajabu, na kuchangia katika kufundisha turathi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), na kufanyia kazi maneno ya bibi Zainabu (a.s) yasemayo: (Wallahi hauwezi kufuta utajo wetu) pamoja na kuangazia turathi za bibi Hauraa, ambapo khutuba hiyo ni miongoni mwa turathi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: