Kamati ya Swidiqah Twahirah (a.s) ya madaktari wa kike chini ya idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake katika ziara ya mwezi kumi na tano Shabani, wamefanikiwa kutoa huduma ya matibabu kwa idadi kubwa ya mazuwaru.
Mjumbe wa kamati hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika wanawake hushiriki kwenye sekta hii ya tiba kwenye kila msimu wa ziara, lakini ushiriki wa ziara hii umekua tofauti, huduma zimetolewa chini ya kivuli cha kamati ya Swidiiqah Twahirah (a.s) iliyo undwa kabla ya muda mfupi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufikia malengo kama yalivyo pangwa na idara ya madaktari wa Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa: “Huduma zimetolewa na wahudumu wa kujitolea ambao ni madaktari wabobezi tofauti pamoja na wauguzi, na kundi la watumishi wa shule za Alkafeel waliofanya kazi ya kuunganisha watu waliokua tayali kujitolea na kuwapa huduma za kijikimu, sambamba na kuhakikisha mgonjwa anaingia katika mikono salama na kupata tiba sahihi anayo hitaji”.
Akabainisha kuwa: “Kazi imedumu kwa muda wa siku tatu mfululizo na walikuwa na vituo viwili, cha kwanza kilikua kinaitwa Ummul-Banina (a.s) kilicho kuwepo katika mlango wa Aljawaad (a.s), na kingine kituo cha Aqiilah (a.s) katika mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Kumbuka kuwa kamati ya Swidiiqah Twahirah (a.s) ya madaktari ipo chini ya idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inaundwa na jopo la madaktari na wauguzi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.