Hospitali ya rufaa Alkafeel inaomboleza kifo cha mmoja wa watumishi wake

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Asubuhi ya Jumamosi (3 Aprili 2021m) imefanya hafla ya kuomboleza kifo cha mmoja wa watumishi wake aliyekufa kwa virusi vya Korona ambavyo alivipata wakati akitekeleza majukumu yake ya uuguzi.

Hafla imefunguliwa kwa ujumbe kutoka kwa mkuu wa hospitali ya Alkafeel Dokta Jaasim Ibrahimi, ambae ameonyesha masikitiko ya kuondokewa na muuguzi hodari, na akatoa pole kwa familia yake na rafiki zake wote.

Katika hafla hiyo pia limesomwa tamko la Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani, linalo husu watumishi wa afya wanaopambana kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, tamko hilo linasema: (Atakaepoteza maisha yake katika kupambana na virusi vya Korona atapata malipo ya Shahidi na atafaulu katika siku ya hesabu…).

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inamchango mkubwa katika kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kupitia kamati maalum zilizo undwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye mikoa tofauti ya Iraq, sambamba na juhudi yake ya kutoa elimu ya afya katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: