Chuo kikuu cha Alkafeel kimechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi wakati wa mitihani

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi wakati wa mitihani ya msimu wa kwanza wa mwaka wa masomo (2020 – 2021), kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona na kufuata maelekezo ya kuhakikisha usalama wa walimu na wanafunzi yaliyo tolewa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Makamo rais wa chuo kikuu Dokta Nawaal Almayali amesema: “Chuo kilianza mapemba kufanya maandalizi ya mitihani hii, kiliweka mkakati unao endana na mazingira ya sasa ya uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona, tuliunda kamati maalum yenye jukumu la kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kuhakikisha mitihani inafanywa katika mazingira salama”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo yaliyo fanywa ni kubaini kumbi za mitihani na kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwa kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, pamoja na kila mwanafunzi kufaa barakoa na kufuata maelekezo mengine ya kujikinga na maambukizi”.

Akafafanua kua: “Uongozi wa chuo chini ya rais wake Dokta Nuusis Dahani, umefuatilia kwa karibu utekelezaji wa masharti ya kujikinga na maambukizi, kwa ajili ya kulinda usalama wa wanafunzi na walimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: