Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika shughuli za siku ya nakala-kale za kiarabu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia maktaba na Daru Makhtutwaat chini ya kamati ya athari na turathi za taifa katika wizara ya utamaduni wa kiiraq, imeshiriki maonyesho yanayo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi na mazingira) ndani ya ukumbi wa makumbusho ya taifa la Iraq.

Maonyesho hayo yamefunguliwa siku ya Jumapili (21 Shabani 1441h) sawa na (4 Aprili 2021m), pamoja na kuangalia namna ya utunzwaji wake na kuzilinda zisiharibike.

Kiongozi wa tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho hayo Ustadh Muhammad Baaqir Zubaidi amesema kuwa: “Hakika ushiriki wa maonyesha haya umefanywa na vituo vitatu vilivyo chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambavyo ni: kituo cha upigaji picha wa nakala-kale na faharasi na kituo cha kukarabati nakala-kale na kituo cha kuhuisha turathi, nakala-kale mbalimbali zimeonyeswa pamoja na vitu vya kihistoria, zikiwemo nakala za Quráni tukufu zilizo andikwa karne ya kwanza hijiriyya hadi karne ya kumi hijiriyya, na vitu vya kihistoria na (maji) yenye miaka (150) iliyopita, pamoja na matoleo maalum ya faharasi za nakala-kale zikiwemo za Atabatu Abbasiyya tukufu na msahafu wa ibun Bawaab na kitabu cha Athari zilizo andikwa kuhusu Imamu kiongozi wa waumini (a.s) pamoja na matoleo mengine ya turathi”.

Akaongeza kuwa: “Vilevile matawi yameonyesha vifaa mbalimbali vinavyo tumika kukarabati nakala-kale na hatua tofauti za kurekebisha nakala-kale hizo na vifaa maalum vilivyopo katika kituo cha kuhuisha turathi, vinavyo tumika kuhakiki nakala-kale zisizo hakikiwa na kuziweka kwenye machapisho tofauti na majarida mbalimbali ya turathi yanayo andika Makala na tafiti za turathi na nakala-kale pamoja na mambo ya kihistoria”.

Akaendelea kusema: “Pamoja na kushiriki katika maonyesho haya kulikua na ugeni maalum wa ofisi katika ufunguzi wa maonyesho, uliofanywa ndani ya ukumbi mkuu wa makumbusho, ulio hudhuriwa na muwakilishi wa waziri wa utamaduni Dokta Naufal Abu Raghiif na mkuu wa athari za turathi Dokta Liith Majidi Hussein, na washiriki wengine kutoka Ataba na vituo vya turathi”.

Kumbuka kuwa hii ni sehemu ya ushiriki wa maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya Iraq, kwa ajili ya kutambulisha kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kulinda turathi na utamaduni, na kuziweka tayali kwa ajili ya kutumiwa na wasomi katika kufanya tafiti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: