Wizara ya utamaduni: Kazi ya kulinda turathi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya inastahiki pongezi

Maoni katika picha
Wizara ya utamaduni na utalii imesisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kamati ya turathi na wizara ya utamaduni.

Hayo yamesemwa wakati muwakilishi wa wizara Dokta Naufal Abu Raghiif alipo tembelea tawi la Ataba linalo shiriki kwenye maonyesho ya siku ya nakala-kale za kiarabu, yanayo fanywa na Daru Makhtutwaat chini ya kamati ya athari na turathi za taifa chini ya kauli mbiu isemayo: (turathi na mazingira) ndani ya ukumbi wa makumbusho ya taifa la Iraq.

Akaongeza kuwa: “Hakika tunaona fahari kwa mahudhurio ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, taasisi yenye mafanikio makubwa katika sekta ya turathi na uhakiki wa nakala-kale hususan katika uibuaji wa urithi huu mtukufu, kazi wanayo fanya inastahiki kujivunia na kupongezwa”.

Kumbuka kuwa tawi la Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha habari na utamaduni linalo shiriki katika maonyesho haya, linamatokea ya tafiti na machapisho ya turathi pamoja na vitu vingine vyenye uhusiano na turathi na vifaa vinavyo tumika kutunzia, muwakilishi wa waziri amesikiliza maelezo kwa ufupi kutoka kwa wasimamizi wa shughuli hizo.

Kumbuka kuwa maonyesho haya yalifunguliwa Jumapili asubuhi mwezi (21 Shabani 1442h) sawa na tarehe (4 Aprili 2021m) yanalenga kuangazia utunzaji wa nakala kale, Atabatu Abbasiyya imewakilishwa na: kituo cha upigaji picha na faharasi na kituo cha ukarabati wa nakala kale na utunzaji wake na kituo cha kuhuisha turathi, wameonyesha mali-kale na vitu mbalimbali vya kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: