Chuo kikuu cha Al-Ameed: Mitihani inafanywa chini ya tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa mitihani ya wanafunzi wake wa chuo ya msimu wa kwanza wa mwaka huu (2020 – 2021) inafanywa katika mazingira ya tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi.

Makamo rais wa chuo Dokta Alaa Mussawi amesema: “Hakika maandalizi ya mitihani yalianza mapema, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, hivyo ukawekwa utaratimu maalumu chini ya usimamizi wa rais wa chuo, ukiongozwa na tahadhari za kujikinga na maambukizi kwa watumishi wetu”.

Akaongeza kuwa: “Mitihani imefanywa kwa kufuata ratiba iliyo pangwa na wizara ya elimu ya juu, na kwa mujibu wa mkakati wa ufanyaji wa mitihani, na utekelezaji wa maazimio ya kamati kuu ya afya ikiwa ni pamoja na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu na kuvaa barakoa, pamoja na kupuliza dawa karibu ya kuanza kila mtihani na baada ya kumaliza”.

Akafafanua kuwa: “Uongozi wa chuo umesisitiza ulazima wa kufuata tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ili kulinda usalama wa wanafunzi, kuna ufuatiliaji wa kuhakikisha kila mwanafunzi anafuata masharti ya kujilinda na maambukizi, na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu”.

Kumbuka kuwa tangu lilipo anza tatizo la virusi vya Korona chuo kikuu cha Al-Ameed kimekua mstari wa mbele kutekeleza masharti ya kujikinga na maambukizi, na kimeunda kamati maalum inayo husika na utekelezaji wa maelekezo ya wizara ya afya, aidha kamati hiyo inajukumu la kupuliza dawa na kuandaa vifaa vyote vya kujikinga na maambukizi sambamba na kutoa elimu kuhusu hatari ya janga hilo na njia za kujikinga.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: