Miswala mipya imetandikwa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya usimamizi wa haram tukufu wametandika miswala mipya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kusafisha na kupuliza dawa kwenye sakafu na kuta zake.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Nizaar Ghina Khaliil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza msimu wa ziara, huwa kuna kazi zinafanywa ndani ya haram tukufu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha miswala (mazulia) na kutandika mapya pamoja na kufanya usafi na kupuliza dawa sehemu zote hadi kwenye dirisha takatifu, watumishi ambao ni masayyid wameshiriki katika kazi hiyo pamoja na baadhi ya watumishi kutoka vitengo tofauti wamejitolea kufanya kazi hiyo”.

Akaongeza: “Kazi hiyo hufanywa usiku baada ya kupungua harakati za mazuwaru, ambapo hufungwa haram tukufu na kutandua mazulia ya zamani, kisha tunapiga deki kuanzia kwenye dirisha takatifu hadi kwenye pambo la sega (twarimah) pamoja na korido nne zinazo zunguka eneo la dirisha, sambamba na kusafisha kuta kwa kutumia vifaa maalum”.

Akaendelea kusema: “Idadi jumla ya mazulia yaliyo tandikwa yamefika (255) yenye ukubwa tofauti, hutandikwa baada ya kuwekwa namba na kubaini sehemu litakapo tandikwa, hii inasaidia kuhakikisha kila zulia linatandikwa sehemu linapo stahiki, haya ni mazulia ya kifahari na yanamichoro mizuri inayo endana na utukufu wa sehemu hii”.

Akasema: “Hali kadhalika tumesafisha dirisha tukufu kwa kutumia vifaa maalum vinavyo saidia kulinda uhalisia wake, kisha tumefukiza na kupuliza marashi yenye ubora mkubwa”.

Kumbuka kuwa tawi la usimamizi wa haram linajukumu la kutoa huduma ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na sehemu ya pambo la dhahabu, na miongoni mwa majukumu yake ni kutandika mazulia ndani ya haram na kusafisha kuta na mapambo yake wakati wote, bila kusahau sehemu za milangoni, taa na viyoyozi, na kila jambo linalo pelekea kuweka muonekano mzuri wa malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: