Maahadi ya Quráni tukufu imeratibu nadwa kwa anuani isemayo (Quráni tukufu na Mahadi)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya nadwa ya Quráni chini ya anuani isemayo (Quráni tukufu na Mahadi), inayo husu tafsiri ya aya nyingi zinazo eleza swala la Imamu Mahadi.

Mtoa mada wa nadwa hiyo alikua ni Shekh Hamidi Jaafi katika Husseiniyya ya As-haabu Kisaa, kwa kufuata tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, kulikua na mada mbili, mada ya kwanza inahusu aya zinazo muelezea Imamu Mahadi (a.f) katika surat Qadr na tafsuri mbalimbali.

Na mada ya pili ilikua inajibu shubuha za wanaokataa kuwepo kwa Imamu, kwa kutumia vitabu vikubwa vya kielimu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni miongoni mwa vituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inalenga kufundisha elimu ya Quráni na kuandaa jamii inayo fanyia kazi mafundisho ya Quráni na sunna na yenye uwezo wa kufanya tafiti za zielimu katika sekta zote za Quráni takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: